Written by 6:04 pm News

Gavana Stephen Sang aachiliwa huru kwa dhamana ya KSh 1 milioni ▷ Kenya News

Mahakama ya Kisumu Jumanne Juni 10 ilimuachilia huru gavana wa Nandi Stephen Sang kwa dhamana ya KSh milioni 1

Gavana Sang alikuwa ameshtakiwa kwa makosa matatu ikiwemo uharibifu wa mali, matumizi mabaya ya mamlaka na uchochezi.

Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, Sang alishtumiwa kwa kuvamia na kuharibu shamba la mimea ya Chai la kampuni ya Kibware akidai shamba hilo lilikuwa limenyakuliwa na mwanasiasa Henry Kosgei.

Habari Nyingine: Mbunge David Sankok amshauri bintiye kuwakimbia wanaume feki

Habari Nyingine: Jamaa akamatwa na kushtakiwa kwa kumtandika mwenye nyumba aliyekuja kudai kodi usiku

Sang alikanusha mashtaka dhidi yake na hata kutaka mahakama isimuhukumu ila aliachiliwa kwa bondi ya KSh milioni 1 na mdhamini wa kiasi hicho au bondi ya KSh 500 pesa taslim.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Tazama habari zaidi hapa TUKO.TV

Source: Tuko News

(Visited 54 times, 1 visits today)