Written by 9:39 pm News

Mchungaji adaiwa kusimamisha harusi baada ya wachumba kula sahani moja ▷ Kenya News

Harusi ya wapenzi wawili kutoka Nigeria inadaiwa kusitishwa na mchungaji baada ya wachumba hao kula sahani moja.

Inakisiwa kwamba, wawili hao walitazamia kufunga ndoa kwa muda wa juma moja lijalo lakini huenda harusi hiyo ikasahaulika kufuatia hatiua hiyo.

Habari Nyingine: Sonko azungumzia picha yake na Passaris wakiwa wamekumbatiana kitandani

Jamaa mmoja kutoka Twitter aliyefahamika kama Realoladele alifichua kwamba wachumba hao walitazamia kufunga ndoa mnamo Juni, 8 2019.

Wapenzi hao aidha walifanya harusi yao ya jadi Juni 7.

Wakati wakifanya harusi ya jadi, wawili hao walipokea ujumbe mfupi wakiarifiwa kwamba harusi yao imefutiliwa mbali.

Habari Nyingine: Je nini hatima ya Jeff Koinange baada ya watazamaji kulalamika kuhusu maadili katika kipindi chake?

Inadaiwa kwamba, mchungaji huyo aliwaadhibu kwa tuhuma za kwenda kinyume na maadili ya imani ya dini wanayoshiriki.

Realoladele alidai kwamba bi harusi mtarajiwa alipandwa na mori na kuangua kilio kutokana na hasara iliyokuwa ikiwakodolea macho kutokana na kuharibika kwa mpango mzima.

“Mamake bi harusi mtarajiwa aliangua kilio huku akigaa gaa sakafuni na kumsihi mtumishi huyo kubadili msimamo wake lakini juhudi zake hazikufua dafu. Hata Yesu Christo hakuwapuuza wenye dhabi kiasi hicho,” alisema.

Aliongeza, juhudi za jamaa wa wachumba hao kumsihi mchungaji huyo kwa pamoja pia hazikufaulu kwani alishikilia msimamo wake.

Hata hivyo, wadau mitandaoni waligadhabishwa na hatua ya pasta huyo na kusema kwamba alikosea kusitisha ndoa yao kwa kisingizio cha maadili ya imani kwani wawili hao walikuwa wamekata shauri kuishi pamoja.

Haya ni baadhi ya maoni yao:

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko News

(Visited 62 times, 1 visits today)