Written by 5:37 pm News

Mtangazaji Annitah Rey adai sio lazima watoto wawatumie wazazi pesa wanapopata ajira ▷ Kenya News

Mtangazaji maarufu Annitah Rey ameibua hisia tofauti miongoni mwa Wakenya baada ya kutoa madai kuwa sio lazima watoto wawatumie wazazi wao pesa wanapopata ajira

Kulingana na Annitah ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha kwamba anamlea mwanawe kwa njia itakikanayo ikiwemo kumpatia elimu bora.

” Sio lazima uwatumie wazazi wako pesa, lilikuwa jukumu lao kukulea, hawapaswi kukuitisha pesa zozote kama njia moja ya kutaka kulipwa,” Annitah alisema.

Aidha, Annitah alidai watoto wengi huwakimbia wazazi wao ama wanawaepuka kwa sababu ya mazoea yao ya kuwaomba pesa kila mara.

Kwa upesi Wakenya walioonekana kukerwa na madai hayo walifurika mitandaoni na kutoa hisia tofauti ;

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Tazama habari zaidi hapa TUKO.TV

Source: Tuko

(Visited 1 times, 1 visits today)