Written by 4:13 am News

Vijana wazua vurugu katika hafla ya kumwombea gavana wa Bomet, Joyce Laboso anayeugua ▷ Kenya News

– Wakazi wa kaunti ya Bomet walitangamana pamoja kwa ajili ya ibada ya kumuombea gavana wao

– Gavana Laboso amelazwa katika hospitali moja jijini London ambapo anapokea matibabu

– Vijana wenye hamaki walitatiza hafla ya maombi na kulazimu viongozi wa kanisa kuondoka kabla ya ibada kukamilika

Hafla ya maombi iliyoandaliwa kaunti ya Bomet kumuombea gavana Joyce Labosa ambaye amelazwa mjini London ilitibuka baada ya vijana wenye hamaki kuitatiza.

Vijana hao walidai kutelekezwa na serikali ya kaunti licha ya kuahidiwa ajira na serikali hiyo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2017.

Maafisa wa polisi walilazimka kufika eneo hilo kutuliza hali ila mambo hayakuenda shwari kwani vijana hao walizidi kuzua vurugu zaidi.

Habari Nyingine: Mwanafuzi wa JKUAT aliyepigwa risasi akiingia Ikulu atoweka kutoka hospitali ya Kenyatta

Habari Nyingine: Viongozi Kisii wapendekeza Matiang’i amrithi Rais Uhuru Kenyatta 2022

Vijana hao walimkashifu naibu gavana wa kaunti hiyo Hillary Barchok na askofu Augustine Rugut kwa kutowajali na kutoa madai ya kuwakwaza mioyo kwenye hafla hiyo.

TUKO.co.ke inafahamu kuwa gavana Laboso amelazwa katika hospitali moja mjini London na anatarajiwa kusafarishwa hadi nchini India kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, haijabainika gavana huyo anaugua ugonjwa upi hadi kufikia wa leo licha ya kulazwa kwa zaidi ya mwezi mmoja hospitalini.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko

(Visited 1 times, 1 visits today)