Written by 11:40 am News

Picha tamu za sherehe ya kuzaliwa ya mama, mpenzi wa Diamond Platinumz ▷ Kenya News

– Mamake Diamond Platinumz, Sandra Kassim na mpenziwe Tanasha Donna walisherehekea siku yao ya kuzaliwa Jumapili Julai 7

– Wawili hao wanashiriki siku zao za kuzaliwa na haya yalithibitishwa na Diamond mwenyewe

– Tayari Diamond na Tanasha wametangaza kuwa wanatarajia mwana wao kwanza ambaye ni wa kiume

Mwanamuziki nyota Diamond Platinumz alimuandalia sherehe nono ya kuzaliwa mamake mzazi Sandara Kassim pamoja na mpenzi wake Tanasha Donna Jumapili Julai 7.

Habari Nyingine: Kampuni ya matatu ya Kileton taabani baada ya utingo wake kudaiwa kuua abiria

Awali, Diamond alitangaza kupitia mitandao ya kijamii kwamba mamake na mpenziwe wanashiriki tarehe moja ya kuzaliwa na kwamba angewaandalia sherehe ya kufana ikizingatiwa ni watu muhimu kwa maisha yake.

Hivyo basi, mamake Diamond na Tanasha walikuwa na wakati mzuri huku wakiwa wamevalia mavazi ya kuvutia kwenye sherehe hiyo.

Habari Nyingine: Rais Uhuru amtaka mwanawe kuoa Mtanzania

Akitoa hotuba yake kwanye sherehe hiyo, Diamond alitangaza kuwa yeye na Tanasha wanatarajia mtoto wa kiume, habari iliyopokelewa vema na wafuasi wake.

TUKO.co.ke iliweza kukusanya baadhi ya picha za sherehe hiyo na bila shaka ni za kupendeza mno.

Habari Nyingine: Kariobangi Sharks vs Everton: Everton wapondwa ugenini

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko

(Visited 67 times, 1 visits today)