Written by 3:58 pm News

Mpenzi wake Willy Paul asimulia alivyomtishia maisha ▷ Kenya News

Mpenzi wake msanii Willy Paul, Susan Mwaniki, amesimulia jinsi ambavyo mwimbaji huyo alimtishia maisha huku akisema atamuua baada ya kushuku alikuwa amemcheza na rafiki yake.

Mwaniki amesema alipitia hali ambayo hajawahi kukutana nayo siku hiyo ambapo Willy Poze alichukua simu yake na kuchokora na ghafla akadai alikuwa amepeana mchuzi wake.

Habari Nyingine: Washukiwa 6 wazuiliwa kuhusiana na wizi wa KSh 72M

Mpenzi wake Willy Paul asimulia Wlly Paul alivyomtishia maiza

Willy Paul amedaiwa kumtishia mpenzi wake huku akisema atamuua. Picha: Willy Paul
Source: Instagram

“Tulikuwa ndani ya gari lake tukielekea nyumbanimkwake Syokimau wakati aliniuliza kama mimi huongea na rafiki yake Kelvin,” Susana alisema.

“Willy Paul alichukua simu yangu na kutafuta nambari ya jamaa huyo kwenye WhatsApp na pia SMSes. Ghafla akawa mkali sana na kuanza kunitishia. Nilijua ni mwenye vurugu, lakini sikujua angenichapa,” alisema.

Susan, ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Kenya, alisema tukio hilo lilifanyika Julai 3.

Habari Nyingine: Majambazi walioiba KSh 72M walilamba kila kitu, watupa masanduku kichakani Kiambu

Msichana huyo alisema mambo yaliharibika zaidi walipofika nyumbani kwani alipata kichapo zaidi huku akitishiwa kuuawa.

“Alinipa kichapo na sikuwa na la kufanya. Nilikuwa nimeona amechapisha picha kwenye Instagram akiwa na bunduki na hivyo kuwa na woga mwingi,” aliongeza mwanafunzi huyo.

“Alisema kuwa ataniuma kwa sababu si mara ya kwanza kufanya hivyo. Usiku mzima alisema nikifikisha asubuhi itakuwa miujiza. Alikuwa akisema hakuna mtu anaweza kupeana tunda lake,”

Binti huyo alipiga ripoti kwenye kituo cha polisi cha Thika.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

(Visited 39 times, 1 visits today)