Written by 11:36 pm News

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Kikuyu Samidoh ahusika kwenye ajali ▷ Kenya News

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Kikuyu Samuel Muchoki, ambaye anajulikana sana kwa jina lake la steji Samidoh, Jumapili, Septemba 8, alinusurika bila majeraha baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabarani.

Samidoh alisema alikuwa kwenye safari ya kuelekea Oljororok wakati ambapi mkasa huo ulitokea na kutatiza safari yake.

Habari Nyingine: Bwenyenye kutoka Mombasa kizimbani kwa kukwepa kulipa ushuru wa KSh 2 bilioni

“Ni vigumu kuelewa vile mambo mengine hufanyika. Asanti Mungu kwa kutulinda,” alisema Samidoh.

“Ilikuwa nihudhurie hafla ya Moses Marite huko Ol jororok Kirima,” aliongeza.

Mashabiki wake alimiminika kwenye ukurasa wake wa Facebook kutoa pole zao na kumtakia siku nyingi duniani ili azidi kuwachangamsha kimziki.

Habari Nyingine: Machakos: Makahaba waandamana na kumtaka gavana kuwapa vifaa vya kazi

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Kikuyu Samidoh ahusika kwenye ajali

Mwimbaji Samuel Muchoki pamoja na mwenzake Joyce wa Mama. Picha: Samidoh
Source: Facebook

Msanii huyo wa benga ameibukia kupendwa sana na mashabiki wake tangu kuondoka katika bandi ya mwimbaji Kamande wa Kioi na kuanza safari yake mwenyewe.

Msanii huyo hapo awali alieleza jinsi ambavyo alilelewa katika maisha ngumu baada ya baba yake kufariki aalipokuwa na miaka mitatu.

Mamake baadaye pia alifariki alipokuwa katika kidato cha kwanza.

Hata hivyo, licha ya changamoto hizo, aliweza kubobea kwenye mziki na pia kujiunga na idara ya polisi wa utawala.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 073248269

Subscribe to watch new videos

(Visited 92 times, 1 visits today)